Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imetoa mikopo yenye thamani ya zaidi Milioni 228 kwa vikundi vya wanawake vijana na walemavu
Akikabidhi mfano wa hundi hiyo leo Desemba 21, 2021 katika ghafla fupi iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Halmasahauri Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amesistiza vikundi hivyo kuhakikisha wanarejesha kwa wakati fedha hizo ili wengine waweze kupewa.
“Fedha hizi za serikali zinatolewa bila riba ili ziweze kuwasaidia na kukuza kipato, tupo tayari kushirikiana na vijana ili kuhakikisha mnakuwa kiuchumi kitu cha muhimu ni kuhakikisha fedha hizi zinarejeshwa kwa wakati ili wengine waweze kupata ,” amesema Dc Sawala
Aidha katika hotuba yake amewasistiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Uviko -19 sambamba na kujitokeza kuchanja chanjo ya ugonjwa huo kwaajili ya kujilinda na kujikinga huku akiwataka kuachana na imani potofu juu ya chanjo hizo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya TandahimbaMhe. Baisa Baisa amesema mikopo hiyo imetolewa na fedha ya mapato ya ndani ambayo ni asilimia 10 ambapo wanawake asilimia 4,vijana asilimia 4 na walemavu asilimia 2
“Mikopo hii nasisi pia madiwani tutaisimamia kwakuwa vikundi hivi vipo katika maeneo yetu pia ni wananchi wetu,ili warejeshe kwa wakati na wengine waweze kukopa,wanaohitaji pikipiki au bajaji hatutawakabidhi mkononi fedha,tutawanunulia a kuwakabidhi nia yetu ni njema kuwa mtumiaji anafanya biashara na analipa marejesho,”amesema Mwenyekiti
Aidha naye Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Tandahimba ndugu Aloyce Massau amesema kuwa idadi ya waombaji imeongezeka kwa kiasi kikubwa ambapo imezidi bajeti kwakuwa jumla ya wote walio omba ilifikia zaidi ya Bilioni tatu kiwango ambacho ni cha juu
Amesema kuwa kiasi cha shilingi 228,509 472 zimetumika kugawa kwa vikundi ambapo shilingi 188,101,872 ni mapato ya ndani na shilingi Milioni 40 ni marejesho ya vikundi jumla hiyo imetumika kugawa kwa vikundi kumi vya wanawake, vijana vikundi kumi ,walemavu vikundi saba na mtu mmoja mmoja watu kumi
“Katika kipindi hiki vikundi vingi viliomba na kufikia zaidi ya Bilioni tatu ya watu wanaohitaji Mkopo,kiwango ambacho ni kikubwa,kwa wale ambao hawajapata kwa vile mwaka wa serikali bado haujaisha watakavyokuwa wanarejesha tutaendelea kutoa mikopo hiyo kwa wale wenye sifa,”amesema Massau
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa