Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amewasistiza mafundi viongozi na wazabuni wa vifaa kutekeleza miradi ya BOOST kwa kuzingatia mpango kazi ili kukamilisha kwa wakati na ubora unaotakiwa
Akishuhudia tukio la kusaini mikataba ya mafundi viongozi na wazabuni wa vifaa kwenye kikao cha Wadau wa Maendeleo Mei 2,2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri Dc Sawala amewapongeza kwa kupata nafasi hiyo ili kuijenga Tandahimba
" Nawapongeza kwa kupata nafasi hii, na asilimia kubwa ya mafundi viongozi ni wanatandahimba,natumaini mtaifanya kazi hii kwa ubora na kwa wakati huku mkizingatia mpango kazi ili ikamilike mapema, kwakuwa miradi hii siyo ya kwanza natumaini mtafanya vizuri zaidi,"amesema Dc Sawala
Aidha amewasistiza waheshimiwa madiwani kuhamasisha wananchi kushiriki katika miradi ambayo inatekelezwa katika maeneo yao sambamba na kuisimamia ili iweze kukamilika kwa wakati
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe. Baisa Baisa amesema muhimu kuweka uzalendo mbele ili kuijenga Tandahimba kwakuwa mafundi viongozi asilimia kubwa ni wanatandahimba
" Kinacho nifurahisha miradi hii inatekelezwa Tandahimba na asilimia kubwa mafundi viongozi na wazabuni ni wanatandahimba Kazi hii tuifanye kwa ushirikiano na ubora, wazabuni ambao mtatengeneza milango msilipue fanyeni kazi zenye ubora ," amesema Mwenyekiti
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imepokea shilingi Milioni 665.1 kutekeleza ujenzi wa miundombinu katika shule za msingi ambapo kwa awamu ya kwanza shule saba zitatekeleza miradi hiyo
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa