Na Kitengo cha Mawasiliano
Mratibu wa Ukimwi Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Ally Sembe amesema kuwa Elimu inaendelea kutolewa kwa jamii na makundi yaliyo kwenye hatari ya kuambukizwa Virusi vya Ukimwi sambamba na ugawaji wa kinga
Amesema hayo Oktoba 31,2022 katika Kikao cha Kamati ya Kudhibiti Ukimwi cha Robo Julai – Septemba 2022 kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano
“Elimu tunayotoa katika jamii inaleta manufaa ambapo masuala ya Unyanyapaa na ubaguzi yamepungua kwa kiasi kikubwa hivyo kuleta mwitio mzuri kwa jamii wa upimaji wa VVU kwa hiari katika vituo vya upimaji,”amesema Mratibu
Aidha amesema kuwa Kuanzishwa kwa huduma ya upimaji wa uwingi wa virusi kwenye damu (HVL) kunafanya wateja kuzingatia dawa za kufubaza maambukizi ya VVU
Katika Kikao hicho Mratibu aligawa Mipira ya kiume (Kondom) 5600 kwa wajumbe wa Kamati hiyo ili waweze kugawa katika maeneo yao hivyo kufanya idadi ya Mipira ya Kiume iliyosambazwa kufikia 88446
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa