Na Kitengo cha Mawasiliano.
Shirika lisilo la kiserikali la ECLAT DEVELOPMENT FOUNDATION limejanga na kukabidhi Shule Mpya Shikizi ya Namindondi Juu yenye Vyumba Vinne vya Madarasa, Ofisi Mbili na Matundu ya Vyoo 16 vyenye Thamani ya Zaidi ya Tsh.Milioni 100 katika Kijiji Cha Namindondi Kata ya Nguja .
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Michael Mntenjele ambae amekuwa Mgeni Rasmi katika hafla hiyo amewashukuru wafadhili hao kwa kuwasaidia watoto waliokuwa wakitembea umbali wa Kilomita 4 kufuata Shule nyingine ya Namindondi akiwasisitiza wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto Shuleni ili wapate Elimu ambayo ni haki yao ya Msingi na kuwakemea baadhi ya wazazi wanaowazuia watoto hasa wa kike kwa sababu zisizo na Msingi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Elimu Wilaya ya Tandahimba Mshamu Bakiri ambae alishirikiana na Wafadhili hao katika kujenga Shule hiyo amewashukuru kwa kuona umuhimu wa kutoa fedha na kujenga Shule hiyo Kwa ajili ya kuunga Mkono Juhudi za Serikali za kuboresha Elimu.
Aidha, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sesthenes Lihende amesema Shule Iko kwenye Mchakato wa kusajiliwa ili Mwezi wa Januari 2025 ianze kutumika Rasmi huku akiahidi kuleta walimu wa Kutosha kwa ajili ya ufundishaji.
Katika Hafla hiyo Viongozi mbalimbali wamehudhuria akiwemo Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Mhe.Katani Katani, Mwakilishi wa Katibu Tawala Wilaya Fransis Mkuti na wengine.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa