Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Mhe. Katani Ahmed Katani amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amekuwa Mstari wa Mbele katika Shughuli za Uhifadhi wa Mazingira akiwa Mfano wa kuigwa na kuongeza kuwa ni vema Tandahimba ikawa sehemu ya Wilaya zinazoongoza katika kutunza mazingira.
Mhe.Katani aeyasema hayo Januari 25, 2024 kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika Shule ya Sekondari Mkonjowano katika Kampeni ya Upandaji miti Kimkoa iliyofanyika Wilayani hapo .
Aidha, Mhe.Katani ameonya ukataji Miti usiofuata Utaratibu na uchomaji wa Miti katika Hifadhi kwani huleta athari za kimazingira ikiwemo ukame na Mafuriko.
"Ndugu zangu tuwekeze katika Kupanda Miti kwa kuwa inafaida kubwa watu wamenufaika na kupata fedha nyingi kupitia Uhifadhi wa Mazingira ikiwemo Biashara ya Hewa Ukaa(carbon Business) "Mh
e.Katani
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa