Na Kitengo cha Mawasiliano
Naibu Katibu Mkuu OR-Tamisemi (Afya) Dkt. Grace Magembe amesistiza miradi ya afya kukamilika kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma katika maeneo yao
Ameyasema hayo leo Julai 27,2022 katika ziara yake Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ambapo ametembelea mradi wa kituo cha afya Kitama ambao unatekelezwa kwa fedha za mapato ya ndani,mradi wa ujenzi wa Nyumba ya watumishi unaotekelezwa eneo la Hospitali ya Wilaya na kituo cha afya Maheha
“Nasistiza miradi hii ikamilike haraka ili wananchi wapate huduma katika vituo hivi lakini pia watumishi wasogee karibu na eneo la kazi,miradi hii ipo nje ya muda hivyo usimamizi uongezeke ili ikamilike,”amesema Dkt Magembe
Aidha amesema kuwa serikali haiwezi kuleta vifaa na watoa huduma katika miradi ambayo haijakamilika lakini pia kuchelewa kwa mradi ni kuchelewesha upatikanaji wa huduma kwa wananchi ambapo hiyo siyo dhamira ya serikali yetu
Naye Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndugu.Robert Mwanawima ameahidi miradi hiyo kukamilika haraka ili wananchi waanze kupata huduma
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa