Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba DCI.Mariam Mwanzalima ametembelea Miradi ya Maendeleo Katika Sekta ya Afya na Elimu inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri hiyo na kusisitiza Kasi iongezeke bila kuathiri ubora wa Miradi hiyo.
Akiambatana na wataalamu wa Halmashauri hiyo Wakiwemo wahandisi DED Mwanzalima amewataka wasimamizi wa Miradi na kamati za Ujenzi kuongeza nguvu katika kusimamia miradi hiyo akitolea mfano wa Madarasa ambayo yanatarajiwa kutumika Mwezi Januari Shule zitakapofunguliwa.
DCI. Mwanzalima ametembelea na kukagua ukamilishaji wa Vituo vya Afya vinne ikiwemo Mihambwe, Maheha, Mambamba, Litehu sambamba na kutembelea Shule ya Sekondari Makondeni, Shule ya Msingi Namahonga na Mkwedu.
Aidha, wasimamizi wa Miradi hiyo wameahidi kutekeleza maagizo yaliyotolewa na kukamilisha Kwa wakati.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa