Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Mussa Gama ametoa wito kwa wazazi na Waleziwa wanafunzi kuhakikisha wanafunzi wanahudhuria shule ili kuepuka utoro sambamba na kuzingatia watoto wanapata chakula shuleni
Ametoa wito huo Septemba 23,2022 kwenye kikao cha wazazi katika shule ya msingi Chikongola na kueleza kuwa jukumu la kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula niletusote ili wanafunzi waweze kusoma vizuri ili waweze kufikia malengoyao
“Mtoto ili aweze kufanya vizuri zaidi darasani anahitaji chakula jukumu hili ni letu wazazi na walezi,utaratibu huu unapunguza utoro wa rejareja kwa wanafunzi wetu,”amesema Mkurugenzi Gama
Aidha amesema kuwa tatizo la utoro wa wanafunzi kwa shule za msingi na Sekondari lipo,wazazi na walezi watawajibishwa pale ambapo hawatahudhuria shuleni
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa