Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkurugenzi Mtendaji Halmasahauri ya Wilaya yaTandahimba Ndg.Mussa Gama ametoa wito kwa taasisi za kifedha kuchangia mfuko wa elimu ili kuendelea kuboresha Elimu Halmashauri ya Tandahimba
Ametoa wito huo wakati akizungumza na wawakilishi wa taasisi za kifedha zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ofisini kwake Februari 8,2023
“Najua tunashirikiana katika masuala mbalimbali lakini kuna mfuko wa elimu ambao una mchango mkubwa katika kusaidia masuala ya elimu ndani ya Halmashauri yetu,wito wangu kwenu ni kuchangia mfuko huu ili uendelee kusaidia Elimu ndani ya Halmashauri yetu,”amesema Ded
Nao wawakilishi wa taasisi zilizohudhuria kikao hicho kwa nyakati tofauti wamempongeza Mkurugenzi kwa kuwashirikisha kuchangia mfuko wa elimu wa Wilaya na wameahidi kutoa ushirikiano katika hilo
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa