Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Maandalizi ya wanafunzi 3656 sawa na asilimia 65 wanaotarajia kuanza kidato cha kwanza mwaka 2021 katika Halamsahauri ya Wilaya ya Tandahimba kwa upande wa miundombinu ya madarasa yamekamilika kwa asilimia 99
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba katika ukumbi wa Mikutano wakati Akitoa tathimini ya hali ilivyo ya madarasa na samani baada ya kufanya ziara ya siku tatu kwa shule 28 za sekondari
Dc Waryuba akiwa kwenye ziara ya kuuangalia madarasa na samani katika sjhule za sekondari
“Tumefanya ziara ya kuona hali halisi ya shule zetu za sekondari upande wa madarasa kwa asilimia 99 tumefanikiwa,nampongeza Mkurugenzi kwa kufanikisha kuna madarasa mawili yapo hatua ya boma yakimaliziwa hatutakuwa na upungufu , ila upande wa meza na viti bado tunauhitaji naamini hili pia Mkurugenzi atalisimamia na wanafunzi wa kidato cha kwanza watasoma katika mazingira mazuri,”amesema DcWaryuba
Dc Waryuba akionyesha kiti na meza vya chuma na kusistiza vitengenezwe vya aina hiyo
Aidha amesema katika ziara hiyo imebainika kuwa kati ya meza3,656 na meza 3,656 zinazohitajika kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza vilivyopo ni meza 1,164 na viti 1,104 upungufu uliopo ni meza 2,492 na viti 2552 ametoa maagizo katika kata ambazo sekondari hizo zipo kuhakikisha wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaporipoti madarasa yawe na samani hizo
Naye Mkurugenzi Mtendaji Said Msomoka ambaye aliambatana na Dc katika ziara hiyo amesema jukumu la samani atalisimamia ili ifikapo January wanafunzi wa kidato cha kwanza wakae katika mazingira rafiki
Dc Waryuba (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji Ndg Msomoka wakiangalia taarifa mbalimbali za shule
“Kwa upande wetu mwaka jana tuliweza kuongeza madarasa zaidi ya 80 ndiyo maana mwaka huu hatujapata changamoto ya madarasa,hivyo nguvu tunaelekeza kwenye samani naamini tutalimaliza ifikapo Januari,”amesema Msomoka
Mkurugenzi Mtendaji ndg Msomoka akimsistiza jambo Mkuu wa shule ya Sekondari ya Mdimba
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa