Pichani: Watumishi wa Mahakama wilayani Tandahimba wakiwa katika picha ya pamoja kwenye kilele cha siku ya sheria
Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe. Sebastan Waryuba amewataka watendaji wa mahakama wafuate maadili ya kazi zao ili kuwezesha shughuli za mahakama kuendeshwa bila viashiria vya rushwa.
Akizungumza siku ya Kilele cha maadhimisho ya Sheria ambayo yamefanyika leo katika viwanja vya Mahakama ya wilaya ya Tandahimba alieleza kuwa watendaji hao wasitoe nafasi kwa wananchi kuwaona ni kikwazo katika kesi zao.
“Watendaji fanyeni kazi kwa uadilifu ili kuepuka mianya ya rushwa, kwa kufanya hivyo mtakuwa mnajenga Imani kubwa kati ya wananchi na ninyi hususani makarani”,alisema Waryuba
Aidha amewaomba wawekezaji kuja kuwekeza katika Wilaya ya Tandahimba kwakuwa maeneo yapo mazuri kwa uwekezaji wa kibiashara kama kauli mbiu ya siku ya sheria inavyohamasisha uwekezaji.
Naye Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Tandahimba Mhe. Joseph Waruku alieleza kuwa mabadiliko ya sera ya mara kwa mara huwa hayawavutii wawekezaji na hivyo kushindwa kuwekeza katika sekta mbalimbali hususan viwanda.
“Sera zinavyobadilika badilika huwa haziwavutii wawekezaji na kuona kuwa kama ni kikwazo kwa upande wao ,lakini sisi kama mahakama tupo katika kipindi cha maboresho ya huduma zetu,”alisema Hakimu Waruku
Hata hivyo Mwenyekiti wa Mawakili wa Kujitegemea Wilaya ya Tandahimba Abdallah Makongoro alibainisha kuwa uwepo wao katika Mahakama kunawezesha wananchi kupata huduma kwa wakati hali inayopelekea kuleta faraja kwa wananchi.
Mamia ya Wananchi wilayani Tandahimba wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa wilaya ya Tandahimba (Pichani hayupo)
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa