Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amepokea madawati 50 yenye thamani ya shilingi Milioni 5 kwa ajili ya shule ya msingi Matogoro
Kaimu Afisa Elimu Msingi bi. Hilda Tamba(kushoto) akiwa pamoja na wanafunzi,wafanyakazi wa benki ya Nmb na mmoja wa walimu wa shule hiyo
Akipokea madawati hayo ambayo amekabidhiwa na Benki ya Nmb tawi la Tandahimba amesema kuwa madawati hayo yatawasaidia wanafunzi kusoma katika mazingira rafiki kwakuwa bado wanauhitaji wa madawati katika shule za msingi
Dc Waryuba akitoa neno kwa kamati ya shule ya msingi Matogoro
“Tunaishukuru Benki ya NMB kwakushiriki katika kuchangia huduma za kijamii,Madawati haya yatapunguza uhaba wa madawati kwa shule yetu na itawaongezea ari wanafunzi kusoma kwa bidii kitu muhimu ni kuhakikisha yanatunzwa ili wengine waweze kuyatumia,”amesema DcWaryuba
Meneja wa Nmb tawi la Tandahimba bi. Julieth Ndazi akimkabidhi Dc Waryuba madawati
Akikabidhi madawati hayo kwa niaba ya Meneja wa Kanda yaw a NMB,Meneja wa benki ya Nmb Tawi la Tandahimba Julieth Ndazi amesema kuwa ni utaratibu wa benki ya NMB kutoa asilimia moja ya faida na kuirudisha kwa jamii ambapo fedha hizo hutumika kutengeneza samani katika sekta ya Elimu,afya na majanga yanapotokea
Meneja wa Nmb Tawi la Tandahimba bi Julieth Ndazi akisoma taarifa fupI kwa Dc Waryuba
“Sisi NMB tupo karibu na wananchi wa Tandahimba kwa kutambua kuwa wateja wetu wakubwa ni wakulima hivyo faida tunayoipata tunairudisha kwa jamii ili kuboresha huduma kwenye sekta ya elimu,afya na majanga pale yanapotokea ndani ya Wilaya,”amesema bi. Ndazi
Madawati 50 ambayo yamekabidhiwa kwa shule ya msingi Matogoro na benki ya Nmb
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba Sosthenes Luhende ameishukuru benki hiyo kwa kushirikiana na Halmashauri katika sekta ya Elimu ambapo kila mwaka hutoa samani kwa shule za Msingi na sekondari
Afisa Elimu Sekondari Sosthenes Luhende akitoa neno kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tandahimba
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa