Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amesema ataendelea kuwakamata wazazi pande zote mbili mara binti wa shule akipatikana na ujauzito ili kukomesha vitendo vya mimba za utotoni na amewataka kuboresha mila zao kwa kuacha kuwafundisha watoto mila potofu
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mambamba na Majengo
Ameyasema hayo wakati akijibu kero ya Hamis Linangwa mkazi wa Ching`ati Kata ya Namikupa aliyehoji kwanini mzazi akamatwe mara mtoto anapopata ujauzito wakati mzazi hausiki
Dc Waryuba amesema mila hiyo ya kuwafundisha watoto wa kike vitu ambavyo vipo juu ya uwezo wao ndiyo inayosababisha watoto kupata ujauzito wakiwa bado shule na kuolewa wakiwa na umri mdogo
Dc Waryuba akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chihangi na Namikupa
“Kuna baadhi ya vipengele katika Mila zenu zinahitaji maboresho,boresheni hii mila ya chikuvelevele ambayo watoto mnawafundisha mambo yanayowazidi matokeo yake ndo mimba za utotoni,sitaacha kuwakamata na kuwachukulia hatua wazazi pande zote mbili na kijana muhusika tena sasa hivi na binti mwenyewe tutamkamata ,”amesema Waryuba
Wakina mama wa kijiji cha Chihangi na Namikupa ambao walijitokeza kumsikiliza Dc Waryuba
Aidha amesema Kata ya Namikupa ni miuongoni mwa maeneo ambayo yapo mpakani wananchi wanatakiwa kutoa taarifa kwa mgeni yeyote ambaye anafika katika maeneo yao ili waweze kumtambua ili kuendelea kulinda amani,usalama na utulivu
Dc Waryuba (katikati) akimsikiliza mwananchi wa kijiji cha Milidu akitoa kero yake
“Wilaya yetu ipo mpakani na nchi ya Msumbiji hivyo mnatakiwa kutoa taarifa endapo mnaona watu msiowaelewa ili tuchukue hatua za haraka,lakini Wilaya yetu ipo salama tuendelee kuitunza amani na utulivu ambao tunao,na tusikubali kuipoteza amani kwa hali yoyote na tumejipanga kisawasawa,”amesema Waryuba
Baadhi ya wataalamu wa Halmashauri kutoka idara mbalimbali wakisiliza kwa makini kero za wananchi
Ziara za Dc Wryuba ni muendelezo wa ziara zake za kutembelea vijijini kusikiliza kero za wananchi na kukagua miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa katika maeneo hayo ambapo hadi sasa zaidi ya vijiji 137 kati ya 143 ameweza kuvifikia na vitongoji zaidi ya 50 kati ya 73 vya Mji mdogo Mahuta na Tandahimba ameweza kuvifikia
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa