Na Kitengo Cha Habari na Mawsiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amezindua zoezi la Ugawaji dawa za minyoo tumbo kwa watoto wenye umri wa kwenda shule ambapo wananfunzi 62726 wanatarajiwa kupewa dawa hizo
Akizundua zoezi hilo katika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ameeleza kuwa viongozi wa dini ndani ya Wilaya wanajukumu la kuwaelewesha wananchi kupitia nyumba za ibada kuhusu zoezi hilo kwakuwa baadhi ya wananchi wana Imani potovu kuhusu dawa hizo
“Zoezi hili linaanza tarehe tisa lakini viongozi wa dini mna jukumu la kuwaambia waumini katika nyumba za ibada umuhimu wa dawa hizi kwa watoto ,mkitusaidia huko katika nyumba za ibada zoezi hili litakuwa rahisi zaidi ,”amesema Waryuba
Aidha amewataka wananchi kutowazuia watoto kupewa dawa hizo kwakuwa hazina madhara ila zina umuhimu katika kuwalinda na minyoo tumbo kutokana na mazingira ya watoto na ulaji wao ambao hawana utaratibu katika mazingira ya shule
“Ugonjwa wa minyoo tumbo unawasumbua watoto kwakuwa ulaji wao kwa umri huo uanakuwa ni wa ovyo hivyo dawa hizi zina umuhimu ili kuwakinga na maradhi ya minyoo tumbo ili waendelee kuwa na afya njema,”amesema Waryuba
Naye Mratibu wa afya ya uzazi na mtoto Hospital ya Wilaya Tandahimba Emily Lutandika amesema kuwa katika zoezi hilo wanatarajia kuwapatia dawa za minyoo tumbo wanafunzi 62726 kwa Wilaya yote ambapo wavulana ni 31731 na Wasichana 30995
Amesema usambazaji wa dawa utaanza rasmi leo ili kuwawezesha itakapofika tarehe 9 walengwa hao ambao ni wanafunzi wa shule za msingi
kuanzia darasa la kwanza hadi la saba waweze kupewa dawa hizo kwa wakati
“Zipo changamoto ambazo tunakutana nazo kwa wazazi kuwakataza watoto wao kutokunywa dawa kwa kuwa na Imani potofu kuwa zinasababisha ugumba dhana amabayo si sahihi ,lakini pia katika ugawaji wa dawa hizi wapo watoto waliopo majumbani 4260 nao watapatiwa dawa hizo,”amesema Lutandika
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa