Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amewataka maafisa ugani kuwa karibu na wakulima katika maeneo yao kwa kuwapa ushauri wa kilimo ili kuongeza uzalishaji wa zao la korosho na mazao mengine ya chakula
Ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa maafisa ugani wa Vijiji na Kata jana katika ukumbi wa mikutano,amesema pamoja na kutoa ushauri maafisa ugani katika maeneo yao wanapaswa kuwa na mashamba ya mfano ili wakulima wajifunze kutoka kwao
Maafisa Ugani wa kata na vijiji kwenye mkutano wa kupanga mikakati ya kuleta mapinduzi ya uzalishaji
Amesema kuwa ili kuweza kuongeza uzalishaji ni jukumu la maafisa ugani kuhamasisha wakulima kutibua mashamba ya korosho ili maji yaweze kuingia kwenye ardhi sambasamba na kuondoa mikorosho iliyozeeka kwa kusimamia ukataji wa kitaalam
Dc Waryuba akiwasistizia maafisa ugani kusimamia kampeni ya ondoa mapori ongeza uzalishaji
“Mikorosho inahitaji maji ya kutosha wahamasisheni wakulima watibue mashamba yao ili maji yaweze kuingia kwa wingi katika mikorosho ili tuongeze uzalishaji na hiki kipindi cha mvua tusisahau mazao mengine wananchi walime mazao ya chakula,hatutaki njaa katika Wilaya yetu,”amesema Dc Waryuba
Mkurugenzi Mtendaji ndg Said Msomoka (kati) akiwa na Mweka hazina Ally Machela(kushoto) na Afisa Kilimo Issa Naumanga kwenye Mkutano na maafisa Ugani wa kata na vijiji
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ndugu Said Msomoka amesema kampeni ya ondoa mapori ongeza uzalishaji italeta mapinduzi katika Halmashauri kwakuwa wakulima wapo tayari kuondoa mikorosho iliyozeeka
Mkurugenzi Mtendaji ndg Said Msomoka akieleza jambo kwa maafisa ugani
“Hii kampeni italeta mapinduzi makubwa katika uzalishaji lakini maafisa ugani wakulima wanawategemea kitaalam nendeni mashambani walipo ili turudi tulipo kiuzalishaji naamini tunaweza tukisimama kila mmoja sehemu yake,”amesema Mkurugenzi
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa