Shamba la mmea aina ya bangi robo ekari ambayo limekamatwa kijiji cha Chaume
Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba ameagiza kung`olewa robo ekari ya mmea aina ya bangi ambayo ameipanda shambani kwake mkazi wa kijiji cha Chaume Said Abdalla (41) na Shahame Saidi (25)
Waryuba amesema mkazi huyo amepanda mmea huo wa bangi kwenye shamba lake ambalo amechanganya na mazao mengine kama vile choroko na mahindi kitendo ambacho ni kinyume na sheria na taratibu za nchi
Mkuu wa Wilaya akionyesha mmea huo kwa baadhi ya wananchi waliojitokeza mahali hapo
“Tunashukuru Jeshi la polisi kwa jitihada zao kwa kushirikiana na wananchi kwa kufanikisha kukamatwa kwa huyu mkulima, Upandaji na utumiaji wa bangi ni kosa la jinai hivyo mmea huu nimeagiza utolewe na tayari zoezi la ung`oaji limeaza na wakazi hawa watachukuliwa sheria inayostahili ili iwe fundisho kwa wengine ,”amesema Waryuba
Aidha amewataka wananchi kupanda mazao ambayo ni halali katika jamii badala ya kujiingiza katika upandaji wa mimea ambayo itakuwa na madhara kwa vijana na kupoteza nguvu kazi ya Taifa
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wakiwawekea mzigo wao wa bangi tayari kwa kuibeba
Naye Mkazi huyo Said Abdallah (41) amejitetea kuwa sababu iliyompelekea kupanda zao hilo ni kutokana na ugumu wa maisha na inamuongezea nguvu akiwa anafanya shughuli za shamba
“Mimi sitarudia tena Mkuu,nilipanda kwasababu ya ugumu wa maisha tuu,na muda mwingine nikinusa majani haya yananisaidia kupata nguvu ya kuendelea na kazi ya kulima,”amesema Abdallah
Mkulima wa shamba hilo wa kijiji cha Chaume Said Abdallah (41) akiwa na mwanae Shahame Said(25)
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa