Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amefurahishwa na mahudhurio ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari baada ya kukaa kwa muda wa miezi mitatu nyumbani kutokana na Homa kali ya mapafu (Covid – 19)
Hilo limebainishwa na Dc Waryuba alipofanya ziara ya kutembelea shule za sekondari na Msingi ili kuangalia mahudhurio ya wanafunzi na hatua zinazochukuliwa kujikinga na Covid – 19 baada ya kurudi likizo ya dharura iliyosababishwa na Covid - 19
Mkuu wa Wilaya Sebastian Waryuba alipotembelea shule ya msingi Tandahimba
“Nimeridhishwa sana na mahudhurio haya ya wanafunzi katika shule za msingi na Sekondari,kwakweli kila shule ambayo nimetembelea asilimia 85 wameripoti shuleni,na kila shule nimeona maji tiririka na sabuni kwa ajili ya watoto kunawa,nimefarijika sana,”amesema Waryunba
Mwanafunzi wa shule ya msingi Tandahimba akinawa maji tiririka na sabuni kujikinga na Covid -19
Aidha ametoa wito kwa walimu wakuu kuhakikisha wanafuatilia walimu wa madarasa ili kuweza kuangalia endapo kuna mwanafunzi mwenye shida yoyote ya kiafya
Naye Mkuu wa shule Sekondari ya Milongodi Donald Mchawa amesema kuwa katika shule yake wanafunzi ambao wameripoti ni asilimia 89 kwa kidato cha kwanza hadi cha nne na walimu wote wameripoti shule
Sekondari ya Milongodi wameweka maji tiririka kwa ajili ya wanafunzi kunawa
“Tangu niwe Mkuu wa shule kwa miaka sita hapa mahudhurio ya wanafunzi kuripoti kwa wingi namna hii sijawahi kuona, nasisi tumejiandaa kuwafundisha na kuwapa mazoezi ambayo yatachangia akili ziwe shule,”amesema Mchawa
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa