Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amekutana na Viongozi wa Vyama vya Siasa wa Wilaya ya Tandahimba kuimarisha Mahusiano na Ushirikiano ili kuendelea kuhamasisha wananchi katika shughuli za Maendeleo.
Akizungumza na Viongozi hao Oktoka 6,2023 Dc Sawala amesema wameruhusiwa kufanya mikutano lakini ni jambo jema kutoa taarifa mapema kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama kwenye eneo la Mkutano.
" Tuendelee kuimarisha mahusiano na.ushirikiano huku tukitambua wote tunajenga nyumba moja ya kuwaletea wananchi wa Tandahimba Maendeleo,Siasa za kistaarabu ni nzuri mnashindana kwa hoja ," amesema Dc Sawala.
Kwa upande wa Viongozi wa Vyama vya siasa wamepongeza hatua ya Mkuu wa Wilaya kukutana nao na wameiomba Serikali ya Wilaya hususan Jeshi la Polisi kutoa ushirikiano wanapohitaji ulinzi wa Jeshi la polisi kwenye Mikutano yao ya hadhara.
Naye Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Tandahimba SP.Kulwa Biteme amewahakikishia Viongozi wa Vyama vya Siasa ulinzi na usalama wakiwa kwenye mikutano yao ya hadhara ambapo amesema muhimu kuzingatia taratibu miongozo na sheria za kufanya mikutano ya hadhara.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa