Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Kanali amezindua zoezi la ugawaji wa viti mwendo kwa watoto wenye ulemavu chini ya miaka 17 ambavyo vimetolewa Hospitali ya CCBRT Dar es salaam
Akizungumza mara baada ya kuzindua ugawaji huo leo Agosti 24,2023 kwenye kituo cha Shule ya Msingi Matogoro ,Dc Sawala amewashukuru CCBRT kwa msaada huo na amewasistiza wazazi kuvitunza
" Nawapongeza CCBRT kwa hatua hii ya kutoa viti mwendo kwa watoto wetu,sisi tunawashukuru lakini wazazi mkavitunze ili viendelee kuwasaidia watoto wetu" amesema Dc Sawala
Naye Thadei Luwumba akisoma taarifa fupi kwa niaba ya Mkuu wa Idara ya Elimu Awali na Msingi amesema kuwa zoezi hilo lilianza Mwezi Juni 2023 la kuwabainisha ambapo watoto 62 wenye ulemavu wa viungo walifanyiwa uchunguzi na baada ya uchunguzi huo watoto 18 wenye ulemavu walibainishwa kuhitaji kupewa viti mwendo
Aidha amesema kuwa viti mwendo hivyo vitatolewa kwa watoto kwenye vituo vya shule ya msingi Matogoro,Luagala na Chikongola
Kwa upande wake mtaalamu kutoka CCBRT Zuwena Abdallah amesesistiza kuwa siyo kila kiti mwendo ni kiti mwendo sahihi kwa aliyekuwa na ulemavu
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa