Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala ametoa wito kwa walimu kutekeleza wajibu wao kila mmoja kwa nafasi yake na kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kuletamadiliko katika Elimu
Amesema hayo Septemba 19,2022 wakatiakisoma hotuba yake katika hafla ya uzinduzi wa Miongozo ya Kuboresha Elimu Msingi na Sekondari katika Uumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Tandahimba
Naye Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Mussa Gama amesema kuwa katika uboreshaji wa Elimu changamoto mojawapo ni mdondoko wa wananfunzi kutomaliza mzunguko wa elimu ambapo zipo sababu mbalimbali zinazosababisha mdondoko ikiwepo utoro
“Miongozo hii ambayo imezinduliwa inatoa majibu nainaelekeza niniyatupasa kufanya,lakini miongozo hii mkiichukua na kuiweka bila kuisoma itakuwani kazi bure na mtafanya kazi kwa mazoea wakati sisi tunataka kufanya kazi kwa ufanisi na tija,”amesema Mkurugenzi
Aidha naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa amepongeza hatua hiyo ambapo ambapo amesema lengo ni kuona Elimu Tandahimba inakwenda mbele kuanzia Elimu Msingi hadi Sekondari
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa