Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amezindua ligi ya Sensa Cup Kata ya Namikupa kwa ajili ya uhamasisha wa Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi 2022
Akizungumza na wananchi ambao walihudhuria uzinduzi wa ligi hiyo Agosti 7,2022 katika kiwanja cha Nachipe Dc Sawala amewasistiza wananchi kushiriki zoezi hilo ambalo lina lengo la kupata takwimu sahihi ambazo zitasaidia katika Mipango ya Maendeleo
"Ligi hii ikaongeze hamasa kubwa ya kila mtu kushiriki katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23,2022 kwa ajili ya maendeleo yetu,"amesema Dc Sawala
Ligi hiyo itahusisha timu kumi na nne za mpira wa miguu kutoka katika vijiji vilivyopo Kata ya Namikupa ambapo inatarajiwa kumalizika Agosti 22,2022 ambapo leo timu ya Namdwani Fc imecheza na Namikupa Fc na kutoka droo ya goli 1-1
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa