Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amezindua Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Halmasahauri ya Wilaya ya Tandahimba ambapo amesistiza kutumia jukwaa hilo kujadiliana fursa na changamoto sambamba na kuweka mikakati ya kujitegemea kiuchumi
Akizindua Jukwaa hilo Machi 2,2023 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba amesema kwamba Jukwaa hilo litaondoa matabaka na kuweza kupata fursa ya kujua sharia ambayo itawasaidia kujua haki zao katika masuala mbalimbali
Aidha ametoa rai kwa viongozi wa jukwaa hilo kusimamia miongozo,taratibu na sharia lengo wanawake waweze kujikomboa kiuchumi sambamba na kushirikiana ili kuweza kufikia malengo yao
Imezindua rasmi jukwaa hili la Wilaya ,jukwaa hili likawaunganishe,muhimu sana mpendane,mshirikiane na kuheshimiana ili kwa umoja wenu muweze kujikomboa kiuchumi,”amesema Dc Sawala
Naye Mratibu wa dawati la Jinsia Halmasahauri ya Wilaya ya Tandahimba Bi.Neema Shungu amesema kuwa uundwaji wa majukwaa uwezeshaji wanawake kiuchumi kuanzia ngazi ya kijiji hadi Wilaya yanakwenda kuamsha ari kwa wanawake kujikwamua kiuchumi
Amesema kwamba uwezeshaji wa wanawake kiuchumi ni nguzo muhimu ili kuhakikisha malengo ya maendeleo endelevu pamoja na malengo ya hamsini hamsini ifikapo mwaka 2030 yanafikiwa
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa