Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amesistiza uwazi na uwajibikaji wa bodi ya mfuko wa Elimu sambamba na kuzingatia taratibu, na sharia za uendeshaji wa mfuko ili uweze kufanya mabadiliko katika Elimu
Amesema hayo Machi 7,wakati wa uzinduzi wa bodi ya Mfuko wa Elimu katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ambapo amesistiza uwazi na kubuni miradi yenye tija ili wananchi wanaochangia mfuko huo waweze kunufaika nao
”Nawaasa baada ya uzinduzi huu bodi mkaziangalie sharia,kanuni ,taratibu na miongozo ili muweze kuusimamia kikamilifu lakini mkabuni na kuibua miradi ya kimaendeleo ambayo itaacha alama yenye tija kwa Halmashauri na Wilay kwa ujumla,”amesema Dc Sawala
Aidha amesema kwamba kwa kutumia mfuko wa elimu tuione Tandahimba juu kielimu,uwezo huo upo na nia ipo pia ametoa rai kwa bodi hiyo kushirikisha wananchi na wadau wengine kwa yale wanayostahili kushirikishwa
Naye Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa ameipongeza bodi hiyo na kuaminiwa na kueleza kwamba matumaini yaliyopo ni kuona mabadiliko katika elimu na kuangalia vyanzo vingine kuliko kukitegemea chanzo kimoja cha Korosho
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa