Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amezindua Baraza la Watoto Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ambapo amesema litasaidia kuwajengea uwezo wa kujiamini kuwa na udhubutu wa kufanya mambo mbalimbali yatakayochangia kufanya vizuri katika Kimasomo pamoja na kuwa viongozi bora wa badae
Akizindua Baraza la Watoto leo Juni 12,2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri, Dc Sawala amesema kuwa lengo la Serikali ni kutimiza azma ya kuwashirikisha watoto katika masuala yanayowahusu kwakuwapatia fursa kujadili na kuamua mambo yanayowahusu
" Nimezindua rasmi Baraza la Watoto la Wilaya ambapo lengo la Serikali ni kuwawezesha watoto kujitambua,kujilinda na kujitetea wanapofanyiwa vitendo vya ukatili na kuwajengea maadili mema na kukuza uzalendo wa Taifa lao ,mimi nawatakia kila lililo jema ,Serikali yenu ya awamu ya sita inawajali,sisi Wilaya tutawasikilizeni," amesema Dc Sawala
Naye Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wialaya ya Tandahimba Ndg.Aloyce Massau akisoma taarifa yake kwa Mgeni Rasmi amesema Mabaraza ya Watoto yameundwa kuanzia ngazi ya kijiji ambapo jumla ya Mabaraza ya Watoto 32 ngazi ya kata na mabaraza 143 ngazi ya vijiji na baraza moja la Wilaya yameundwa
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Ramadhani Chimale amesema watazingatia muongozo katika utekelezaji wa majukumu yao sambamba na kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya watoto
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa