Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba amewataka watendaji wa Kata na Maafisa Maendeleo ngazi ya kata kuhakikisha siku 16 za kupinga ukatili wanatumia kwa kutoa elimu katika maeneo yao
Ameyasema hayo Novemba 25,2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri wakati akizindua Siku 16 za kupinga ukatili ambapo amesistiza kila Kata iweze kuhakikisha inatoa elimu ili kuzuia vitendo vya Ukatili
“Leo tunaanza rasmi siku 16 za kupinga ukatili wito wangu kwenu Watendaji Kata wote 32 na Maafisa Maendeleo wa Kata muhakikishe siku hizi 16 mnatoa elimu kwa jamii ya kupinga vitendo vya ukatili,”amesema Dc Sawala
Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba itatoa elimu kwa jamii sambamba na kufanya kongamano la wadau mbalimbali Disemba 6,2022 ambapo Kauli mbiu ya mwaka huu ‘Kila Uhai unathamani Tokomeza Mauaji na Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto’
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa