Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amewataka wakandarasi kuzingatia Mpango kazi katika kutekeleza miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kumi (10) vya madarasa ili kukamilisha miradi hiyo kwa wakati
Amesema hayo Oktoba 12 wakati akifungua kikao kazi cha wasimamizi ambao ujenzi wa vyumba vya madarasa unafanyika katika maeneo ya ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri
‘Tunamshukuru Mhe.Rais kwa kutupatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kumi,zingatieni mpango kazi tuliojiwekea ili madarasa yakamilike kwa wakati na ubora unaotakiwa,wakandarasi wekeni mafundi wa kutosha,”amesema Dc
Naye Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg. Mussa Gama amesema tayari hatua za awali zimefanyika katika maeneo ambayo utekelezaji wa madarasa utafanyika ambapo ni shule ya sekondari Tandahimba,Mndumbwe na Kwanayama
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa