Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe Kanali Patrick Sawala amewataka makatibu wa vyama vya ushirika ( amcos) ambao wamepewa dhamana na Serikali ya kugawa pembejeo katika maeneo yao kufanya kazi hiyo kwa uadilifu
Amesema hayo Mei 30,2023 kwenye kikao cha Kamati ya Pembejeo ya Wilaya ambapo kimepitia mwongozo wa usambazaji na mfumo wa ugawaji wa pembejeo za ruzuku msimu wa mwaka 2023/2024 ili kujenga uelewa wa pamoja
DC Sawala amesema kuwa Serikali imegawa pembejeo hizo bure kwa wakulima ili kuwapunguzia gharama ambapo watasimamia zoezi la ugawaji ili liweze kukamilika kwa ufanisi
Kwa upande wake Kaimu Meneja Mipango ya Kilimo Bodi ya Korosho Tanzania Ndg.Juma Yusuph ameeleza kuwa tayari pembejeo zimeanza kusambazwa ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imeanza kupokea pembejeo hizo kupitia Chama kikuu cha Ushirika Tanecu
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa