Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amewataka mafundi viongozi katika miradi ya Elimu na Afya kuongeza ili kukamilisha miradi hiyo kwa wakati
Dc Sawala (wa pili kulia) akipima ukubwa wa darasa katika shule ya sekondari Mweminaki,wa kwanza kushoto Katibu Tawala Wilaya Juvenile Mwambi,Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Mussa Gama(wapili kushoto)
Dc Sawala akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ndugu Mussa Gama na wakuu wa Idara na Vitengo ameyasema hayo alipofanya ziara ya kukagua miradi hiyo mwishoni mwa wiki ambayo Serikali imetoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wake
“Miradi hii nahitaji ikamilike kwa wakati,mafundi viongozi ongezeni nguvu ya mafundi ili twende na kasi tukamilishe kwa wakati,naamini muda ambao tumejiwekea kukamilisha miradi hii tutafanikiwa,”amesema Dc Sawala
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Sawala akisistiza jambo kwa mafundi wa kituo cha afya cha Tarafa ya Mihambwe
Naye Mkurugenzi Mtendaji ndugu Mussa Gama amewasistiza mafudi kuhakikisha wanafanya taratibu za malipo mara wanapomaliza hatua moja ili kupata malipo yao kwa wakati muafaka
Mkurugenzi Mtendaji ndg Gama (wakwanza kushoto)akipitia nyaraka za mradi wa vyumba vitano vya madarasa shule ya sekondari Michenjele
“Mafundi hakikisheni mnakamilisha taratibu za malipo mara unapomaliza hatua moja kwa kuwa Serikali ina utaratibu wake kwenye malipo siyo unamaliza leo unataka na fedha siku hiyo hiyo ni ngumu,fanya utatibu mapema ili unapomaliza kazi hiyo unapata na fedha yako unaendelea na hatua inayofuata,”amesema Mkurugenzi
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imepata shilingi Bilioni 1.76 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 82 kwa shule za sekondari,na shule shikizi vyumba 6 ,pia imepokea shilingi Milioni 750 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya katika Tarafa tatu fedha zote zimetolewa na Serikali ya awamu ya sita
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa