Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amewasistiza Wakuu wa Shule za Sekondari kusimamia Taaluma ili kuongeza ufaulu sambamba na kusimamia nidhamu na maadili ya wanafunzi kujenga Jamii bora .
Amesema hayo leo Septemba 29,2023 kwenye kikao cha Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari(TAHOSSA) kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Mtwara kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
" Mkasimamie Taaluma kwenye maeneo yenu ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi, lakini pia mkasimamie nidhamu na maadili ya wanafunzi , ili kuendelea kuimarisha mila na desturi za Kitanzania huku mkiwasistiza kusoma kwa bidii na msisite kutoa taarifa za utoro wa wanafunzi ili hatua za kisheria zichukuliwe kuzuia mdondoko wa wanafunzi ," amesema Dc Sawala.
Aidha amewasistiza kusimamia taratibu na miongozo ya utoaji wa adhabu kwa wanafunzi huku akitoa wito kwa walimu kushirikiana na kuepuka makundi ya wao kwa wao katika maeneo yao ya utendaji ambapo pia amewapongeza kwa kusimamia upatikanaji wa chakula shuleni.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari (TAHOSSA) Mkoa wa Mtwara Mwl.Twaha Chitipu amesema pamoja na kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Umoja wao wa TAHOSSA lakini pia wamejadili na kupeana Mikakati ya usimamizi bora wa shule hasa wakilenga kuinua Taaluma na ufaulu
Kikao cha TAHOSSA Mkoa wa Mtwara kimefanyika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ambapo Jumla ya Wakuu wa shule za Sekondari 140 kati ya 171 wa Mkoa wa Mtwara wameshiriki katika kikao hicho.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa