Na Kitengo cha Habari na Mawasailiano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amewataka vijana kushiriki katika shughuli za maendeleo hususan kilimo na miradi inayoendelea katika maeneo yao
Ameyasema hayo leo Juni 23,202 wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mihambwe kuhusu masuala mbalimbali ikiwa pamoja na kusikiliza kero zao ambapo kabla ya kikao hicho alifanya mkutano na viongozi wa dini wa kata hiyo
Viongozi wa dini kata ya Mihambwe wakimsikiliza Dc Sawala(hayupo pichani)
“Vijana mshiriki katika shughuli za maendeleo msiwaachie wazee na akina mama waende shambani peke yao hii siyo sawa,lakini pia mshiriki katika shughuli za maendeleo ambazo zinafanyika katika maene yenu kama vile ujenzi wa vituo vya afya,hii ni miradi yenu ushiriki wenu ni muhimu,”amesema Dc Sawala
Wananchi wa Kata ya Mihambwe wakiwa katika Mkutano wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya (hayupo pichani)
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuendelea kudumisha amani katika maeneo yao sambamba na vijana kushiriki katika ulinzi shirikishi kwa kuanzisha sungusungu ili kuimarisha ulinzi na usalama wa maeneo lakini pia amewahamasisha wananchi kushiriki Sensa ya watu na makazi Agosti 23,2022 kwa maendeleo ya Wilaya na Taifa kwa ujumla
Naye Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndugu Mussa Gama amewahimiza wananchi kuunda vikundi ili wapate mikopo ya asilimia 10 ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu ili kuweza kukuza kipato
Ndugu.Mussa Gama Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba akieleza jambo kwa wananchi wa Mihambwe
Amesema kuwa mikopo hiyo haina riba hivyo jukumu kubwa ni kuhakikisha wanao pata mikopo irejeshwe kwa wakati ili wengine nao waweze kupata
Aidha Mkurugenzi amewaeleza wananchi wa kata hiyo kuwa ukarabati wa shule ya msingi Ruvuma ambayo ni miongoni mwa shule tisa ambazo miundombinu yake iliharibiwa na mvua utaanza hivi karibuni
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa