Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala ametoa siku saba hadi kufikia Jumatatu Januari 23,2023 wazazi na walezi wasiowapeleka wanafunzi wa kidato cha kwanza,walisajiliwa darasa la kwanza na awali hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao
Amesema hayo Januari 17,2023 wakati wa ziara ya ufuatiliji wa maendeleo katika shule za sekondari ambapo timu tatu za viongozi wa Wilaya zikiongozwa na Dc zinapita kata hadi kata shule hadi shule kuangalia hali ya uripoti wa wanafunzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
“Watendaji wa Kata ,vijiji na wenyeviti katika maeneo yenu hakikisheni wanafunzi wanaotakiwa kuripoti shule wakaripoti shule natoa siku saba hadi jumatatu asiyeripoti hatuakali za kisheria zichukuliwe kwa wazazi na walezi wa wanafunzi,”amesistiza Dc Sawala
Aidha katika ziara hiyo amesistiza upatikanaji wa chakula shuleni kwa wanafunzi wote sambamba na kuhakikisha hakuna mdondoko au utoro kwa wanafunzi hususan wanafunzi wa sekondari
“Mkakati wa Wilaya wa kila shule kulima mazao ya chakula uendelee ili wanafunzi wapate chakula shuleni,uongozi wa kata hakikisheni mnapata orodha ya wanafunzi watoro ili wahudhurie shule,mdondoko huu wa wanafunzi usiwepo katika maeneo yetu,”amesema Dc
Kwa upande wa madiwani wa kata ambazo zimetembelewa wameahidi kushirikiana na uongozi wa kata zao ili wanafunzi waripoti shule,ziara hiyo ya siku tatu imeanza Januari 17-19,2023 ambapo shule zote zitatembelewa
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa