Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala ametoa rai kwa Wajane wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba kutumia fursa zilizopo kuinua kipato ili kuboresha maisha yao sambamba na kuchangia maendeleo ya Wilaya na Taifa kwa ujumla
Amesema hayo katika Kongamano la Wajane ambalo limefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Juni 22,2023 ambapo wamejadili masuala mbalimbali yanayowahusu wajane
" Pamoja na changamoto zinazowakabili wajane lakini pia tumieni fursa zilizopo katika Wilaya yetu ili kuinua kipato na kuboresha maisha yenu,ipo mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Halmashauri mnaweza kutumia fursa hiyo pia," amesema Dc Sawala
Siku ya Wajane Duniani huadhimishwa kila mwaka Juni 23 ambapo Kauli mbiu ya mwaka 2023 " Wezesha Wajane kwa Teknolojia Bora Kuwainua Kiuchumi"
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa