Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala akiwa na Kamati ya Usalama Wilaya (KU)pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Ndg.Mussa Gama na Wakuu wa Idara na Vitengo wametembelea Ujenzi wa vyumba kumi vya madarasa ambao unatekelezwa kwa gharama ya Tsh.Mil.200 ikiwa ni maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza2023
Akikagua ujenzi wa vyumba hivyo NovembaDc Sawala amezipongeza kamati kwa ushiriki wao katika miradi hiyo lakini pia amewasistiza mafundi viongozi kuhakikisha wanakamilisha madarasa hayo kwa wakati
“Niwapongeze Kamati za Ujenzi kwa kuendelea kusimamia ujenzi wa vyumba vya madarasa lakini pia nawasistiza mafundi viongozi kuongeza kasi ili tukamilishe kwa wakati lakini kwa ujumla nawapongeza,”amesema Dc Sawala
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ilipokea fedha kiasi cha Tsh Mil.200 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa ikiwa ni maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023 ambapo ujenzi huo unaendelea
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa