Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amewataka wanafunzi wa darasa la saba kuongeza jitihada kwenye masomo ili waweze kufanya vizuri kwenye mitihani yao na kuendelea na Elimu ya sekondari
Ameyasema hayo leo Julai 15/2021 wakati alipotembelea shule ya msingi Amani na kueleza kuwa wasikubali kushawishiwa kutofanya vizuri katika masomo kwa sababu yoyote ile ili waweze kufikia malengo yao
“Natumaini mmejiandaa vizuri,ongezeni juhudi katika masomo usikubali mtu yoyote akushawishi ufanye vibaya katika masomo ili usiendelee na masomo,huyo anataka ndoto zako za mafanikio zisifanikiwe ,”amesema Dc Sawala
Aidha Dc Sawala ameongea na walimu wa shule hiyo na kuwasistiza kuendelea kutimiza majukumu yao ili wanafunzi waweze kufanya vizuri kwenye masomo na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa madarasa yenye mitihani
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ndg Yusuph Ulaya amesema walimu wamejipanga kiufundishaji na wanaendelea kutekeleza majukumu yao kama kawaida ,kwa madarasa yenye mitihani wameweka utaratibu unaofaa
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Walimu ,Bi Logisiana Mbawala amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa kuwatembelea na kuongea nao wamemuahidi kuendelea kutekeleza majukumu yao ipasavyo ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa