Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amesistiza usimamizi wa pamoja na uwajibikaji kila mmoja kwa nafasi yake ili kuleta ufanisi katika kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani ambayo yanatekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo
Amesema hayo kwenye Kikao cha Wadau wa Maendeleo wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Juni 7, 2023 kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri
Katika kikao hicho wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba waliwasilisha taarifa ya Hali ya makusanyo ya mapato ya ndani,Hali halisi ya upatikanaji wa chakula mashuleni na Hali ya usafi wa mazingira ambapo wadau wametoa mapendekezo na ushauri wao
Aidha DC Sawala akifunga kikao hicho amesema kuwa mapendekezo na ushauri ambao umetolewa na wadau kwa lengo la kuboresha uzingatiwe na mikakati bora ya utekelezaji ifanyike ili kuongeza mapato ya ndani na upatikanaji wa chakula ufikie asilimia 100 kwa shule zote za Msingi na Sekondari sambamba na usafi wa mazingira
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa