Na.Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala Septemba 19,2023 ametembelea na kukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Chuo Cha VETA kinachojengwa katika Kata ya Kitama na kuwasisitiza wasimamizi wa Ujenzi huo kuongeza Kasi ya Ujenzi ili kikamilike kwa wakati na Ubora.
Chuo Cha VETA kinachojengwa Kata ya Kitama kinatarajiwa kuwa Mkombozi kwa Vijana wa Wilaya ya Tandahimba na Maeneo Mengine Nchini kupata ujuzi na Maarifa ya kufanya kazi za Kujiajiri na kuajiriwa mara baada ya kuhitimu.
Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba ilipokea Fedha kutoka Serikali kuu kiasi cha Tsh.Bilioni 1.4 kwa ajili ya Ujenzi wa Chuo Cha VETA kinachotarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Februari 2024.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa