Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amesema hatua kali itachukuliwa kwa yoyote atakebainika kuuza pembejeo zinazotolewa na serikali kwa wakulima katika vyama vya msingi
Ameyasema hayo wakati akizungumza na wazee wa Wilaya ya Tandahimba katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba,amesistiza kuwa pembejeo hizo zimetolewa na serikali ili kumsaidia mkulima kupuliza mikorosho kuongeza uzalishaji
“Serikali ina nia njema kwa wakulima lakini wapo watu siyo waamifu wananchukua pembejeo kwenda kuuza,atakayebainika hatutaweza kumvumilia tutamchukulia hatua kali na vyama vya msingi zingatieni kuwa pembejeo hizi ni kwa ajili ya wakulima ambapo idadi yao mnayo,”amesema Dc Sawala
Katika mkutano huo Dc Sawala amezungumzia masuala ya afya,kilimo,ushirika,Elimu,mikopo ya vikundi na ulinzi na usalama,akizungumzia elimu amesema kuwa jamii inatakiwa kusimama pamoja kukomesha utoro na kuwasistiza watoto kuhudhuria shule ili waweze kupata matokeo mazuri
“Naamini tukishirikiana tutapandisha ufaulu wa watoto wetu kuanzia shule za msingi hadi sekondari,najua baadhi ya wazee mnaishi na wajukuu msiwaache wakae nyumbani wasistizeni umuhimu wa elimu,”amesema DcSawala
Aidha katika suala la Kilimo na ushirika amesitiza wananchi kuendelea kulima mazao mchanganyiko na kuongeza zao la ufuta kuwa zao la kibiashara kukuza kipato pia amesistiza viongozi wa vyama vya msingi kuwa waaminifu
Dc Sawala ameendelea kuwahimiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote zinazotolewa na Wizara ya Afya nchini dhidi ya ugonjwa wa korona sambamba na kuendelea kulinda amani na utulivu ndani ya Wilaya
Naye Katibu wa Wazee Wilaya ya Tandahimba ndugu Rashid Kapera amesema kuwa mkutano huo umeleta taswira mpya kwa wazee na wananchi wa Tandahimba kwa pamoja kwa ushirikiano maendeleo yataendelea kuimarika
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa