Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amesema ameridhishwa na utekelezaji wa afua za lishe ngazi ya kata
Ameyasema hayo leo Julai 7,2022 katika kikao cha Tathmini ya utekelezaji wa afua za lishe ngazi ya kata katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri
Watendaji wa kata wakiwa katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa afua za lishe
“Nawapongeza sana kata zote kwa kusimamia jukumu la lishe katika maeneo yenu na kupata alama asilimia mia,hapo mmetekeleza majukumu yenu,mmeitendea haki jamii mnayoingoza na nafasi zenu za usimamizi,”amesema Dc Sawala
Amesema kuwa Watoto wenye lishe bora na afya bora wana uwezo mzuri katika masomo yao na hivyo kutengeneza kizazii bora ambacho kinaweza kusimamia rasilimali za nchi yetu
“Mmefanikiwa kusimamia Watoto wetu wasipate udumavu na utapiamlo kwa kusimamia afua za lishe katika maeneo yenu,ongezeni jitihada pia muwatembelee akina mama wajawazito waliopo katika maeneo yenu,”amesema Dc Sawala
Naye Dkt.Joselyne Kalikawe Mratatibu wa Lishe Wilaya ya Tandahimba amesema kuwa katika Kata zote 32 utekelezaji wa afua za lishe zimefanyika kwa asilimmia mia moja(100%)
Mratibu Lishe Wilaya ya Tandahimba Dkt.Joselyne Kalikawe akifafanua jambo kwa watendaji Kata
Mratibu ameendelea kuwasistiza wazazi,walezi kuhakikisha wanazingatia lishe bora kwa Watoto lkn pia kutoa ushirikiano ili wanafunzi waendelee kupata chakula shuleni kwa asilimia mia moja
Aidha naye Mtendaji wa Kata ya Mkoreha Anifa Shankupa amesema kuwa wataendelea kusimamia afua za lishe katika kata zao ili kuepuka udumavu na utamialo kwa Watoto
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa