Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya yaTandahimba Mhe Kanali Patrick Sawala amesema kuwa anaridhishwa na maendeleo ya operesheni ya Kitaifa ya anwani za makazi ambayo inaendelea ndani ya Wilaya
Ameyasema hayo kwenye ziara yake inayoendelea katika kata zote 32 zilizopo ndani ya Wilaya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na maazimio ya Wilaya na Mkoa katika sekta ya kilimo,elimu na operesheni ya anwani ya makazi
Dc Sawala katika ziara hiyo anapokea taarifa na kukagua hali ya usaili wa wanafunzi wa darasa la awali na kidato cha kwanza,hali ya udahili kwa kidato cha kwanza 2022,hali ya chakula shuleni,mikakati ya kupandisha ufaulu,uwepo wa mashamba ya mazao ya chakula na alizeti kila shule,utekelezaji wa miradi katika kata husika na operesheni ya anwani za makazi
“Naridhishwa kabisa na zoezi hili la anwani za makazi ambalo linaendelea ndani ya Wilaya yetu,kila ninapopita naona kazi imefanyika vibao vimewekwa na namba zimeandikwa kwenye nyumba inanipa faraja sana ,nachukua nafasi hii kuwapongeza viongozi kuanzia wenyeviti wa vitongoji hadi wa kata kwa ushirikiano wenu,natumaini tutakamilisha zoezi hili kwa wakati muafaka,”amesema Dc Sawala
Aidha amesema kuwa hali ya chakula shuleni inaridhisha kuanzia shule ya awali hadi sekondari japokuwa kuna baadhi ya maeneo hawapati wanafunzi wote na ametoa maagizo kuhakikisha wanafunzi wote wanapata chakula shuleni,lakini pia amepongeza shule kwa kuanzisha mazao ya vyakula na mazao ya biashara katika maeneo yao ambayo yatasaidia wananfunzi kujifunza kazi za kilimo na shule kupata chakula
“Kuna mikakati ambayo tuliazimia katika vikao vyetu nafarijika kuwa mnaitekeleza,katika suala la kilimo endeleeni kuwaelimisha wakulima waweze kulimia mashamba yao ya korosho ili maji yaweze kuingia vizuri ili kuongeza uzalishaji lakini katika miradi bado inachelewa chelewa hakikisheni inakamilika kwa wakati,”amesema Dc Sawala
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba anaendelea na ziara ya kutembelea kata zote 32 zilizopo Wilaya ya Tandahimba
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa