Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amepiga marufuku uuzaji na ununuzi wa mihogo mikavu( Makopa) ili kujikinga na upungufu wa chakula ndani ya Wilaya ya Tandahimba
Amesema hayo Agosti 24,2023 kwenye Mkutano wa Mwaka wa kawaida wa baraza la madiwani ambapo amewasistiza madiwani kwenda kuwahimiza wananchi kutunza chakula wanachopata kwakuwa kuna upungufu wa chakula
" Hakuna kibali ambacho kinatolewa kwa wanunuzi kwenda kununua makopa vijijini tangu mwaka jana ,akikutwa mtu ananunua huko vijijini hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake,ni marufuku uuzaji na ununuzi wa makopa ndani ya Wilaya ya Tandahimba,na madiwani mkalisimamie hilo kwenye maeneo yenu," amesema Dc Sawala
Aidha amewasistiza madiwani kwenda kusimamia ukusanyaji wa mapato katika maeneo yao ,kudhibiti utoro wa wanafunzi , kusimamia upatikanaji wa chakula shuleni , kuwahimiza wananchi kulima mazao mchanganyiko na kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ikamilike kwa wakati
Hata hivyo amewataka Watendaji wa Kata kuhuisha daftari la wageni katika maeneo yao ili kuimarisha ulinzi na usalama
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa