Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amepiga marufuku ngoma za usiku na kueleza kuwa zinachangia wanafunzi kupata ujauzito kabla ya wakati wao na kushindwa kuendelea na masomo
Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Mihambwe na amesema kuwa jukumu la wazazai ni kuhakikisha wanafunzi wanahudhuria shule ili waweze kufikia malengo yao na kutoruhusu utoro wa reja reja kwa wanafunzi
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala akizungumza na wananchi wa Kata ya Mihambwe
“Marufuku ngoma za Usiku kwenye Wilaya ya Tandahimba kwa sasa,sikatazi mila na desturi ila usiku hapana,kwakuwa wanafunzi wetu wanapata jauzito huko kwenye ngoma ngoma ambapo wanakutana na mafataki,tena ukibainika umempa mwanafunzi mimba hakuna majadiliano ni mahakamani sharia inasema kosa hilo ni miaka thelathini jela tena mimi natamani wangechapwa na viboko,kwakuwa wanakatisha ndoto za wanafunzi wetu,”amesema Dc Sawala
Aidha Dc Sawala katika mkutano huo amewasistiza wananchi kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao,kuendelea kuchukua hatua dhidi ya UVIKO-19 na kupata chanjo ambayo inapatikana katika vituo vya serikali, kulima mazao mchanganyiko na kuongeza jitihada zao la ufuta ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja lakini pia Taifa kwa ujumla
Wananchi wa kata ya Mihambwe wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Sawala (Hayupo Pichani)
“Nawapongeza wananchi kwa jinsi ambavyo mnashirikiana kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarika,lakini pia naendelea kusistiza kuwa kila mgeni anayekuja katika kijiji taarifa zake zichukuliwe kwenye madaftari ya wakazi ambayo yapo kuanzia ngazi ya vijiji na vitongoji,”amesema Dc Sawala
Naye Mkurugenzi Mtendaji Halmasahauri ya Wilaya ya Tandahimba ndugu Mussa Gama akizungumza na wananchi wa Kata ya Mihambwe amesema kuwa ushiriki wa wananchi katika miradi ya maendeleo ni muhimu kwakuwa wao ni wahusika wakuu wa miradi hiyo katika maeneo yao
Mkurugenzi Mtendaji ndg Gama akizungumza na baadhi ya wananchi na kamati ya mradi ambao walifika kushiriki mradi wa vyumba vya madarasa Sekondari ya Michenjele
“Nawaomba mshiriki katika miradi hii ya madarasa na vituo vya afya ,fedha ipo lakini mkishiriki gharama ambazo zingetakiwa kulipwa zinabaki kwenye kijiji kwaiyo kituo kikikamlika zile fedha zinaweza kutumika kwa kuongeza dawa au kujenga nyumba ya m ganga,”amesema Mkurugenzi
Mkurugenzi Mtendaji ndg Gama akijitambulisha kwa wananchi wa kata ya Mihambwe
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa