Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amesema kuwa anwani za makazi zina umuhimu mkubwa ikiwemo kuboresha huduma za kijamii na amewasistiza watendaji kusimamia zoezi hilo ili liweze kukamilika kwa wakati
Ameyasema hayo leo Februari 16,2022 wakati akifungua kikao kazi cha watendaji wa kata,vijiji na maafisa tarafa kwnye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ili kuwajengea uwezo wa kutekeleza zoezi la anwani za makazi
“Niwaombe watendaji mkatimize wajibu wenu katika kutekeleza jukumu hili kwa wakati Kuna faida nyingi sana za anwani za makazi ikiwemo kuboresha huduma za kijamii na nyingine nyingi hivyo likikamilika kwa wakati itarahisisha shughuli nyingine,”amesema Dc Sawala
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmasahauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndugu Mussa Gama amesema kuwa yale ambayo wawezeshaji wameelekeza katika kikao hicho wakayazingatie ili yaweze kuwasaidia kukamilisha kazi hiyo kwa wakati
‘Naamini zoezi hili tutafanikiwa kukamilisha kwa wakati na kila mmoja atayatekeleza yale ambayo tumekubaliana ili tukayasimamie na kuleta mafanikio chanya ,”amesema Mkurugenzi
Naye Mwenyekiti wa kamati ya anwani za makazi ndugu Nasibu Namkuna amewaeleza kuwa ili waweze kufanikisha zoezi hilo ushirikiano kati ya mwenyekiti wa kitongoji,mtendaji wa kijiji na mtendaji wa kata unatakiwa uwe mkubwa ili kuweza kufikia malengo
Nao Watendaji wa kata kwa nyakati tofauti wamesema kuwa kikao hicho kimewajengea uwezo wa kutekeleza jukumu hilo kwa ufasaha na wakati katika maeneo yao
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa