Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala ametoa wito kwa wananchi wa Tandahimba kuanza kutumia Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Tandahimba ambalo limeanzishwa ili kurahisisha upatikanaji wa huduma karibu na wananchi
Amesema hayo Januari 20,2023 wakati akikagua Ofisi ya Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya Tandahimba ambapo amepongeza jitihada za kufanikisha ofisi hiyo ambayo itarahisisha upatikanaji wa huduma karibu na wananchi
“Wananchi tutumie Ofisi hii ya baraza la Ardhi na Nyumba iliyopo hapa kwetu,nawapongeza mliosimamia kukamilika kwa ofisi hii ambayo itarahisisha upatikanaji wa huduma karibu na wananchi ambao awali walikuwa wanapata huduma hiyo Mkoani Mtwara na hivyo wengine kuacha haki zao zikipotea kutokana na umbali,”amesema Dc Sawala
Aidha amewasistiza wajumbe wa baraza hilo kusimamia haki ili wananchi waendelee kupata huduma bora
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa