Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amekabidhi vifaa mbalimbali kwa Watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Mjimpya Maalum iliyopo kata ya Tandahimba
Akikabidhi vifaa hivyo Leo Juni 14,2022 shuleni hapo ametoa wito kwa wazazi na walezi wenye Watoto wenye mahitaji maalum kuacha kuwaficha nyumbani badala yake wawapeleke shuleni hapo ili wapate haki yao ya msingi ya elimu
“Nimeleta vifaa hapa kwa watoto wetu wenye mahitaji maalum wajue kuwa tunawapenda na tunawathamini sana kwasabaabu wana haki sawa na Watoto wengine ,”amesema Dc Sawala
Aidha amewapongeza walimu wa shule ya mjimpya maalum kwa jitihada wanayoifanya ya kuhakikisha watoto hao wanapata elimu bora sambamba na elimu ya kujitambua ambayo inawasaidia katika shughuli zao za kila siku
Naye Mwalimu Sharifa Machemba kwa niaba ya Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo amemshukuru Dc kwa vifaaa hivyo ambapo amesema vitatumika kama vilivyokusudiwa
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa