Na Kitengo cha Mawasiliano.
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe Kanali Patrick Sawala amekabidhi pikipiki 13 zenye thamani ya Tsh.Mil.30.4 kwa Maafisa Ugani wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Tanecu.
Akikabidhi pikipiki hizo leo Disemba 15,2023 Dc Sawala amewasistiza Maafisa Ugani kuwafikia wakulima kwenye maeneo yao na kuwapa elimu ili kuongeza uzalishaji wenye tija.
"Pikipiki hizi zikafanye kazi iliyokusudiwa ambayo ni kuwafikia wakulima kwenye maeneo yao na kuwapa elimu huku mkizingatia Sheria za Usalama barabarani mnapoendesha vyombo hivyo vya moto," amesema Dc Sawala.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Tanecu Mohamed Mwing'uku amesema kuwa pikipiki hizo zimetolewa kwa Maafisa Ugani 13 ambapo saba (7) wa Tandahimba na sita (6) wa Newala.
Aidha kwa upande wao Maafisa Ugani wameshukuru na kuahidi kutumia pikipiki hizo kwa kazi iliyokusudiwa.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa