Na Kitengo cha Mawasiliano.
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amefika kuona na kuwapa pole Wanafunzi katika Shule ya Msingi Litehu ambako Vyumba viwili vya Madarasa vimeezuliwa na Kubomoka baada ya Mvua kubwa iliyoambatana na Upepo kunyesha mapema leo .
Aidha, DC Sawala amewaona baadhi ya Wanafunzi waliopata majeraha madogo na hali zao zimeimalika baada ya kupata matibabu.
Hata hivyo jitihada mbalimbali zimefanyika ikiwemo kuwatafutia Wanafunzi hao mazingira Mengine ya kusomea.
Sambamba na hayo DC Sawala ameagiza kasi ya Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa vinavyojengwa Shuleni hapo iongezeke haraka ili Wanafunzi warejee kusoma kama ilivyo kuwa awali.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa