Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala akiwa pamoja na Kamati ya Usalama Wilaya na baadhi ya Wakuu wa Idara na vitengo amefanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa,matundu ya vyoo na shule mpya ikiwa na jumla ya shilingi Mil.665.1 fedha kutoka Serikali Kuu kupitia mradi wa BOOST
Ziara hiyo imefanyika leo Juni 26,2023 ambapo ametembelea na kukagua miradi hiyo inayotekelezwa katika shule ya msingi Amani,Mjimpya,Chikongola,Michenjele, Mihambwe, Majengo na shule mpya inayojengwa Mambamba
Miradi hiyo ipo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji ambapo Dc Sawala amewasistiza Fundi Viongozi kuhakikisha inakamilika kwa muda uliopangwa
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa