Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amefanya Mkutano wa hadhara katika Kata za Nambahu na Mkonjoano Kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kata hizo Leo Machi 4, 2024 .
Katika Mkutano wa hadhara Nambahu DC Sawala amewasisitiza Wananchi kuendelea kuamini Viongozi na kutoa changamoto zozote zinazojitokeza ili zipatiwe ufumbuzi wa haraka kwa Maendeleo yao na sio kusubiri mambo yanaharibika .
Miongoni mwa hoja zilizowasilishwa na wananchi hao ni pamoja na kutaka kujua Miradi inayoibuliwa kwa Nguvu za wananchi inakamilishwaje na Halmashauri sambamba na uhakika wa upatikanaji wa pembejeo za Kilimo kwa Wakulima.
Ziara ya Mkuu wa Wilaya Kata kwa kata inaendelea Jumatano Machi 6, 2024 katika Kata za Tandahimba, Miuta, Malopokelo na Kitama.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa