Na Kitengo cha Habari na Mawasilano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amesema utaratibu wa kuwapima wanafunzi wa kike ujauzito uanze rasmi katika shule zote ndani ya Wilaya
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanali Patrick Sawala akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani
Ameyasema hayo jana Septemba 7,2021 kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Tandahimba
Madiwani wakiwa kwenye kikao
“Naagiza rasmi utaratibu wa kuwapima mimba watoto wakike uanze rasmi katika shule zetu zote ndani ya Wilaya lakini natoa wito wazazi na walezi kutoa ushirikiano mara inapobainika mwanafunzi amepewa mimba ili hatua za kisheria zichukue mkondo wake,”amesema Dc Sawala
Wakuu wa Idara na Vitengo wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani
Aidha katika taarifa yake ameelezea masuala mbalimbali ikiwemo afya,elimu,kilimo na ushirika,ulinzi na usalama,maji,usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoendelea katika maeneo mbalimbali ndani ya Wilaya
Kamati ya Ulinzi na usalama wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndugu Mussa Gama akijibu swali la papo kwa papo la Mhe.Njawala Njawala diwani wa kata ya Mnyawa,amesema Halmashauri imejipanga kusimamia na kutekeleza miradi kwa wakati
Mkurugenzi Mtendaji ndg Mussa Gama akijibu swali la papo kwa papo kutoka kwa madiwani
“Nikuondoe hofu Mhe. Njawala mimi na timu yangu tumejipanga kuisimamia miradi inayotekelezwa kuwa inakamilika kwa wakati ili wananchi wapate huduma,”amesema ndg Gama
Aidha naye Meneja Wakala wa Barabara Vijijini (Tarura) Wilaya ya Tandahimba Mhandisi Peter Mliya amewaomba madiwani kuwa wavumilivu ili fedha iliyopatikana ipelekwe katika maeneo ambayo tayari yapo kwenye mpango
Meneja wa Tarura Wilaya ya Tandahimba Mhandisi Peter Mliya akijibu maswali ya madiwani ya papo kwa papo
“Nafahamu kuna barabara korofi lakini wananchi wasichote mchanga barabarani kwakuwa wanasababisha mashimo na kuzidisha ubovu,tutakarabati baadhi lakini tuna mpango wa kujenga barabara km 4 kwa lami,barabara zingine tutaziweka kwenye bajeti ijayo,”amesema Mhandisi
Viongozi wa vyama vya siasa wakifuatilia kikao cha baraza la madiwani
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa