Na Kitengo cha Mawasiliano.
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Michael Mtenjele ametembelea na kukagua Miradi ya maendeleo inayotarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru 2024 na kutoa maelekezo kwa ajili kuboresha Miradi hiyo huku akisisitiza hamasa kwa Wananchi ianze mapema.
Katika ziara hiyo DC Mtenjele ameongozana na Kamati ya Usalama ya Wilaya pamoja na wataalamu mbalimbali ambapo wametembelea Miradi ikiwemo ya Maji, Elimu, Barabara , mradi wa Ufugaji wa Kuku wa Vijana yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 3.2 ambapo Mwenge wa Uhuru 2024 unatarajia kuizindua na mingine kuwekwa jiwe la Msingi.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa